-
Peagas inaendelea na maongezi na uongozi wa Ngome Saccos Ltd., inayotoa huduma ya akiba na mikopo kwa Jeshi la Ulinzi la Wananchi (JWTZ), kujadili jinsi ya kushirikiana katika ununuzi na upimaji wa viwanja maeneo mbali mbali Tanzania kwa ajili ya wanachama wa Saccos hiyo. Peagas inakaribisha taasisi zingine za ukopeshaji zenye hitaji la viwanja vilivyopimwa kwa ajili ya wanachama na wateja wao.
-
Inakadiriwa kuwa zaidi ya asilimia 70 ya wakazi wote wa Jiji la Dar es Salaam wanaishi kwenye maeneo yaliyojengwa holela na yenye msongamano mkubwa. Aidha hali hii imewalazimisha baadhi ya wananchi wengine kujenga sehemu za mabondeni na hivyo kuhatarisha usalama wa maisha na mali zao wakati wa mvua za masika.
-
Tanzania imejaliwa kuwa na ardhi kubwa na ya kutosha kwa kila mwananchi kuweza kumiliki kipande cha ardhi kwa ajili ya shughuli za kiuchumi na kijamii. Kwa ukubwa wa nchi unaokadiriwa kuwa kilomita za mraba 947,000, kila Mtanzania anaweza kumiliki takribani ekari tatu.
-
Pamoja na kwamba Tanzania ina Wizara nzima inayoshughulikia masuala ya Ardhi, ina Chuo Kikuu kishiriki kinachoshughulikia masuala ya Ardhi tu na kuna Idara za Mipango Miji katika kila Halmashauri na Mabaraza ya Miji, hali ya makazi ya wananchi inazidi kuwa mbaya siku hadi siku. Uhaba mkubwa wa viwanja vilivyopimwa umewalazimisha wananchi wengi kujenga makazi kwenye maeneo yenye msongamano mkubwa wa watu.
-
Serikali, imefanya mapitio na kurekebisha Matangazo ya Serikali kuhusiana na Mji Mpya wa Kigamboni ambapo eneo la Mpango limepunguzwa kwa kuondoa kata tatu ambazo ni Pembamnazi, Kisarawe II na Kimbiji. Kwa maeneo yaliyobakia kwenye mradi, wananchi wa Kigamboni wana fursa ya kushiriki katika uendelezaji kwa kutumia njia zifuatazo: 1. Mwananchi mwenyewe kuwa mwendelezaji katika eneo lake kwa kuzingatia Mpango 2. Mwananchi kulipwa fidia au kuuza eneo lake kwa mwekezaji kwa hiari yake kwa kuzingatia bei ya soko 3. Mwananchi anaweza kuingia ubia na mwekezaji kwa kutumia ardhi yake kama mtaji.





New Projects